Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

MAONESHO ya 48 ya Biashara ya Kitaifa ya Dar es Salaam maarufu kama sabasaba yanatarajia kutengeneza ajira za muda zipatazo 11,712 huku watembeleaji wakifikia 353,201.


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,Exaud Kigahe alisema hayo jana Dar es Salaam na kuongeza kuwa ufunguzi rasmi wa maonesho hayo itakuwa Julai 3, katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa  na mgeni rasmi atakuwa Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi akiwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan.

Kigahe alisema kauli mbiu ya maonesho hayo ni Tanzania mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji  ikilenga kuonesha Dunia kubwa serikali ya awamu ya sita ipo tayari  na inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara na wawekezaji wa Ndani na nje ya nchi kufanya biashara na kuwekeza katika  sekta mbalimbali za uzalishaji ikiwemo sekta ya Viwanda,kilimo,teknolojia,uwekezaji na Utalii.

Alisema  maonesho ya mwaka huku yatakuwa ya aina yake ambayo yamejikita katika teknolojia ya Hali ya juu,ubunifu na matumizi ya akili mnemba (AI).

Alisema  kutakuwa na jumla ya washiriki 3846 ambapo washiriki wa Ndani ni 3433,kampuni za Ndani sekta binafsi ni 3286,Wizara nane,mikoa minne,halmashauri 30 na Taasisi za umma 105,nchi za nje 26 na kampuni za nje 413.

Alisema kwa mwaka jana 2023 kulikuwa na jumla ya washiriki 3500 ambapo wa Ndani walikuwa 3233,washiriki wa nje 267,nchi za nje 19,watembeleaji 300701 na ajira 11687.

Alizitaja nchi za nje zilizothibitisha kushiriki ni pamoja na Korea,Uturuki,India,Japan,Singapore,Syria,Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE),Msumbiji,Indonesia,Mauritius,Oman,Misri,Iran,Pakistani,Rwanda,Comoro,Zambia,Ethiopia na Kongo.

Alisema nchi ngingine ni Ghana,China,Urusi, Italia, Uganda,Kenya na Zimbabwe.

Alisema nchi nyingi zinakuja kuonesha teknolojia mpya za mashine mbalimbali ambazo ni zile zinazohitajika na Watanzania katika kuanzisha Viwanda vikubwa,vya kati na vidogo.

"Niwaombe wafanyabiashara wa ndani ya nchi kutumia fursa hiyo kujifunza Kwa ajili ya kuongeza uzalishaji,ubora wa bidhaa pamoja na kupanga wigo wa masoko ya bidhaa zao,"alisema.

Alisema  katika maonesho hayo kutakuwa na siku maalum ya nchi saba zinazoshiriki kwenye maonesho hayo ambazo mi China,Japan,Korea,Iran,Misri,Urusi na India.
Kigahe alisema pia kutakuwa na programu ya sabasaba  urithi wetu,programu za mikutano ya ana kwa ana,siku za kampuni zinazojumuisha sekta mbalimbali ambazo zimeandaliwa Kwa kushirikiana baina ya sekta binafsi na sekta ya umma.

" Lengo la siku hizo za kampuni ni kuwezesha wafanyabiashara wa kitanzania kupata fursa ya masoko ya nje," alisema na kuwataks watanzania wenye vikundi vya ujasiriamali,kampuni,taasisi za umma na binafsi kushiriki kwenye maonesho hayo kwa kuwa ni Jukwaa muhimu sana la kukutana wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kujifunza teknolojia mbalimbali za maarifa ya kisasa ya uzalishaji,ufungashaji na usambazJi wa bidhaa,kupataasoko ya ndani na nje pamoja na ajira