Habari
Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Zanzibar ni sehemu muhimu ya kuwakutanisha wafanyabiashara Mbalimbali kutoka ndani na nje ya Nchi.

Waziri wa Viwanda na Biashara wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Seleman Jafo amesema Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Zanzibar ni sehemu muhimu ya kuwakutanisha wafanyabiashara
Mbalimbali kutoka ndani na nje ya Nchi.
Ameyasema hayo Januari 05,2025 Zanzibar wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya 11 ya Biashara ya Kimataifa Dimani ambapo Dkt.Jafo amesema Maonesho hayo ni jukwaa la Wafanyabiashara kukutana kupeana taarifa mbalimbali pamoja na kuonesha bidhaa walizonazo na hatimae kuchagiza uchumi wa Taifa na mtu mmojammoja na kujemga uelewa wa jinsi bishara na uwekezaji unavyofanyika.
Aidha Dkt.Jafo amezipongeza Taasisi zilizopo mwenye maonesho hayo kwa kuwa tayari kuwasaidia Wafanyabiashara na kwa kutumia mifumo ya kidigitali ili kurahisisha sajili mbalimbali za ufanyaji biashara.
Vilevile ameziagiza Taasisi kuwa mstari wa mbele katika kuwasaidaia Wafanyabiashara na kuacha kuwa kikwazo kwa wafanyabiashara ili kuwasaidia katika shughuli zao.
Pia Dkt.Jafo amewahamasisha Wafanyabiashara kutumia Masoko ya nje ikiwemo masoko la ya AEAC,AGOA, SADC na AfCFTA
Vilevile amezipongeza Serikali zote mbili za Tanzania Bara na Tanzania Visiwani kwa kuweka Mazingira mazuri kwa wafanyabiashara na kufanya kazi zao pamoja na kuwa mstari wa mbele katika kusikiliza changamoto za wafanyabiashara.
Nae Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Fatma Mabrouk Khamis amesema kuwa Maonesho hayo yamehudhuriwa na Washiriki zaidi ya 400 kutoka nchi mbalimbali za ukanda wa Afrika Ulaya na Asia.
Maonesho hayo ni moja ya Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayotarajiwa kuadhimishwaJanuari 12,2024 yenye kauli mbiu “Miaka 61 ya Mapinduzi :Amani Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu.