Habari
Mazungumzo kati ya Waziri na Wafanyabiashara wanaouza AfCFTA

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mb.) amekutana na kuzungumza na Wafanyabiashara wanaouza bidhaa kupitia Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika AfCFTA kuhusu upatikanaji wa mikopo ya kuimarisha mitaji kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa bidhaa bora kwa wingi na kukuza biashara ili kutumia fursa za AfCFTA kikamilifu Januari 9, 2024 Ofisi ndogo za Wizara, Dar es Salaam.