Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Mhe. Charles Mwijage ametoa siku 5 kwa waliopitisha makontena zaidi ya 100 wakajisalimishe.


Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage ametoa siku 5 kwa waliopitisha makontena zaidi ya 100 wakajisalimishe ili kulipa adhabu ya asilimia 85 ya mzigo waliopitisha bila kukaguliwa. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji ameyasema hayo katika kikao chake na waandishi wa habari kilichofanyika Wizarani, jijini Dar es salaam. Mhe. Waziri amesema TBS wanatakiwa kukagua mzigo unaoingia nchini kwa lengo la kusimamia na kukagua bidhaa ili kulinda wafanyabiashara, walaji na kuhakikisha Viwanda vinafanya kazi vizuri kwa kuzingatia ubora wa Viwango.