Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Mhe. Charles Mwijage, atembelea ujenzi wa kiwanda cha Vigae cha kampuni ya (TwyFord Tanzania Cereramics).


Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amepongeza jitihada zinazofanywa na muwekezaji wa kampuni TwyFord Tanzania Cereramics,kwa ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza vigae “Tiles” katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani. Waziri Mwijage, amesema hayo alipotembelea na kukagua maendeleo ya awali ya eneo, litakalojengwa kiwanda hicho cha kutengeneza vigae “Tiles” kitakachotoa ajira kwa watanzania zaidi ya elfu mbili katika mfumo rasmi,na ajira elfu nne zisizo rasmi. Waziri Mwijage aliongeza kuwa,” bidhaa hizi pia zitauzwa katika nchi majirani kama Zambia,Malawi, DRC,Rwanda, Burundi,Uganda na Jamhuri ya watu wa Afrika Kati na kusafirishwa nje ya bara. Aidha Waziri Mwijage alisema kuwa kiwanda hicho kitumike vizuri na kutoa wito kwa watanzania kutumia fursa zitakazo patikana katika mradi huo zitumike kwa faida ya kila mmoja, “Serikali ya kijiji itambue maeneo yake ili kusaidia kuharakisha maendeleo ya eneo hili ambapo kiwanda kinafanya shughuli zake”alisema Mwijage.