Habari
Mhe. Kigahe (Mb) ashiriki Kikao cha kamati ya kudumu ya bunge ya bajeti

Naibu Waziri Mhe. Exaud Kigahe (Mb) ashiriki kikao cha kamati ya kudumu ya bunge ya bajeti kilichofanyika katika ukumbi wa Msekwa tarehe 4 Juni, 2021 ,
Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na wabunge waliopo katika kamati ya bajeti, kilisikiliza taarifa za utekelezaji wa majukumu za taasisi ya TEMDO, CARMATEC na TIRDO zilizowasilishwa na wakuu wa taasisi husika.
akifungua kikao Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya bajeti Mhe. Daniel Sillo Baran ambaye ni Mbunge wa Babati Vijijini alimkaribisha Naibu Waziri Mhe. Exaud Kigahe ili kutoa neno la utangulizi kabla ya kuanza kwa kikao na baadaye wakuu wa taasisi walianza kwa kuelezea taarifa ya utekelezaji wa majukumu katika taasisi zao pamoja na changamoto zinazowakabili.
Waheshimiwa wabunge baada ya kusikiliza taarifa za taasisi walitoa michango yao ya kuishauri serikali na kushauri taasisi husika kuongeza ubunifu na tija katika kuwasaidia wananchi hasa walioko vijijini ambao ndio wahitaji wakubwa wa huduma zao.
Aidha wajumbe wa kamati walishauri taasisi hizi ambazo kwa kiasi kikubwa zinajihusisha na utafiti na ubunifu wa teknolojia zinapaswa kupewa bajeti ya kutosha kwani shughuli wanazofanya zina tija kubwa kwa taifa letu hasa katika kuelekea uchumi wa viwanda, pia wameshauri serikali kupitia taasisi ya TIRDO kubuni teknolojia ya TAX STAMP ya TRA ili itumike katika kurekodi bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu ili kuongeza mapato ya kodi kwa serikali.
Akifunga kikao hicho Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya bajeti Mhe. Daniel Sillo Baran ameishukuru wizara ya viwanda na biashara kwa kuitikia wito wa kamati na kuja kufanya wasilisho zuri ambalo limekuwa na tija kwani wabunge wengi wa kamati walikuwa hawafahamu mambo mengi yanayofanywa na taasisi hizi, Aidha amewashukuru wajumbe wa kamati kwa michango yao ambayo itakuwa chachu ya mafanikio katika sekta ya Viwanda na Biashara.