Habari
Mikataba na wawekezaji wa Mradi wa ECT Cargo unaojihusisha na usafirishaji na Uhifadhi
Jafo(Mb) ameliagiza Shirika la Maendeleo Tanzania (NDC) kupitia mikataba na wawekezaji wa Mradi wa ECT Cargo unaojihusisha na usafirishaji na Uhifadhi wa Mizigo kutoka nchi mbalimbali ndani ya siku 45 ili kuhakikisha Serikali kupitia NDC inanufaika na Uwekezaji huo.
Ameyasema hayo alipotembelea Mradi huo kwa lengo la kuona maendeleo ya ufanyajj kazi na uwekezaji wake leo Februari 15,2025 Jijini Dares Salaam.
Dkt.Jafo amesema kuwa licha ya kodi inayolipwa kwa Serikali katika Uwekezaji huo pia Serikali kupitia Shirika hilo la Maendeleo linanufaika kutokana na umiliki wa eneo lenye mradi huo.
Aidha Dkt.Jafo amewapongeza wawekezaji hao katika hatua wanazochukua za kuongeza wigo wa uwekezaji wa eneo hilo wa zaidi ya Bilioni 17 pamoja na kutoa rai kwao kuendelea kushirikiana na Serikali katika Uwekezaji ili Serikali ibufaike na rasilimali zake.
Naye Mkurugenzi wa Shirika hilo Dkt.Nicholaus Shombe amesema wamepokea maagizo hayo na watahakikisha Shirika hilo linafanya marekebisho kwa muda walipangiwa pamoja na kuweka usimamizi mzuri ili Serikali kupitia Shirika hilo pamoja na wawekezaji wananufaika.
Pia amesema Sera ya Shirika hilo ni kuendelea kushirikiana na wawekezaji mbalimbali ili kuhakikisha Serikali inanufaika ikiwa ni pamoja na upatikaji wa ajira kwa Watanzania.