Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Waziri Jafo Athibitisha Dhamira ya Serikali Kuboresha Soko la Kariakoo.


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo (Mb) amesema Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara itaendelea kutengeneza Mazingira mazuri na bora kwa Wafanyabiara wa Soko la kariakoo pamoja kufungua fursa zaidi kwa Wawekezaji katika soko hilo.

Dkt. Jafo amebainisha hayo wakati wa Hafla ya Utoaji wa Tuzo za Kariakoo Business Award 2025 zilizofanyika Juni 1,2025 katika Ukumbi wa Mlimani city Jijini Dar es Salaam.

Aidha Dkt.Jafo amesema Tuzo hizo ni kuwatambua Wafanyabiashara bora katika Soko hilo la Kariakoo ikiwa ni kuunga Mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuweka Misingi mizuri ya Kibiashara ili kufungua milango kwa Wafanyabiashara hao.

Waziri Jafo amesema katika kutengeneza fursa za ajira zaidi nchini Serikali imeweka vipaumbele katika kukuza ufanyaji wa biashara ili kuongeza ajira nchini pamoja na miundombinu inayochangia ukuaji wa biashara ikiwemo Umeme na barabara.

Vilevile Dkt. Jafo ameushukuru Uongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara katika Soko la Kariakoo kwa Ushirikiano na Wizara katika kuhakikisha kutatua changamoto za Wafanyabiashara katika Soko la Kariakoo.