Habari
Waziri Jafo: Viwango House kuwa Kitovu cha Ubora Afrika ya Kati.
Waziri Jafo: Viwango House kuwa Kitovu cha Ubora Afrika ya Kati.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo ( Mb)amesema Serikali inataka kuhakikisha viwango vinazingatiwa na wanataka nchi iendelee kuheshimika kwa upande wa viwango na maabara inayojengwa ni kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Amezungumza mbele ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb), wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi lililofanyika Juni 4, 2025 Dkt. Jafo ametumia fursa hiyo kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo na miongozo yake ya kuhakikisha Taifa linazidi kupata maendeleo.
“Mhe. Waziri Mkuu, umefanya jambo bora kuweka jiwe la msingi katika jengo hili linalojengwa Dodoma kwa gharama ya Sh bilioni 25.3 na linaendelea kwa mafanikio makubwa, likiwa na viwango vya juu vya ubora na litakuwa la mfano,” alisema Dkt. Jafo.
Aidha, ameeleza kuwa ujenzi wa maabara kubwa ya kisasa unaendelea kwa kasi ili kuondoa changamoto ya kusafirisha sampuli kwenda Dar es Salaam, na maabara hiyo itakuwa bora zaidi katika ukanda wa Afrika ya Kati.