Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

WAZIRI KAPINGA ANADI FURSA ZA UWEKEZAJI NCHINI QATAR


📌lengo ni kuongeza mauzo na uwekezaji kwenye viwanda vya kuongeza thamani ya malighafi;

📌ujumbe wa Tanzania wakutana  na makamu wa kwanza wa chama cha wafanyabiashara na wenye viwanda nchini Qatar;

📌Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba asifu kazi nzuri inayofanywa na Wizara ya viwanda.

Doha, Qatar 

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, ambae yuko nchini Qatar kwa ziara ya kiserikali amesema,Tanzani ina fursa nyingi za kufanya uwekezaji na biashara na nchi ya Qatar hususani kwenye viwanda vya kuongeza thamani.

Mhe Kapinga aneyasema hayo wakati wa mkutano na makamu wa kwanza wa chama cha wafanyabiashara na wenye viwanda nchini Qatar na kuongeza kuwa, mikakati ya Serikali ya kuongeza mauzo ya bidhaa za Tanzania katika soko la Qatar, sambamba na kuvutia uwekezaji wa Qatar nchini, hususan katika viwanda vya kuongeza thamani ya malighafi zinazopatikana Tanzania uko palepale.

Amesema kazi  kubwa inayofanywa na WIzara ya viwanda na Biashara ni kuhakikisha kunakuwa  na mazingira wezeshi ya wawekezaji kuwekeza Tanzania.

Awali akitoa wasilisho kwenye mkutano huo  mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Mwigulu Nchemba na Mhe Mohammed bin Ahmed  bin Twar Al Kuwar, Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE, Ndugu Efraim Mafuru, amesema 
 Tanzania na Qatar, zina fursa za kuongeza mauzo ya bidhaa za Tanzania katika soko la Qatar, pamoja na uwezekano wa kutumia Qatar kama lango la kufikia masoko mapana ya Ghuba. 

Mikakati hiyo pia inalenga kutumia kikamilifu fursa zinazotokana na nafasi ya Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), pamoja na fursa za kibiashara zinazotokana na mahusiano ya Tanzania na nchi za Ghuba.

Mhe. Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na TANTRADE na TISEZA, TPSF na TNCC, kuandaa na kusimamia jukwaa la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Qatar .

Jukwaa hilo linalenga kuwaunganisha wafanyabiashara na wawekezaji wa Qatar na fursa halisi za biashara na uwekezaji zilizopo Tanzania, pamoja na kuwezesha majadiliano ya moja kwa moja kuhusu maeneo ya uwekezaji, uzalishaji, kuongeza thamani ya malighafi na upanuzi wa masoko.

Aidha, Dkt. Mwigulu ameelekeza Wizara kuchukua hatua za haraka kuwaalika QCCI nchini Tanzania, sambamba na kuandaa makongamano ya kibiashara, semina kibiashara mikutano ya fursa za  uwekezaji, majadiliano ya kisekta, kwa lengo la kujenga ushirikiano wa karibu na endelevu kati ya sekta binafsi za Tanzania na Qatar.