Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

WAZIRI KAPINGA ZIARANI NCHINI QATAR KUSHIRIKI ZIARA YA KIKAZI YA WAZIRI MKUU


📍 Doha, Qatar

📌 Kuiwakilisha sekta ya Viwanda na Biashara katika kutangaza na kuendeleza fursa za uwekezaji nchini Tanzania

📌 Kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Qatar kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Salvio Kapinga, amewasili nchini Qatar kushiriki ziara ya kikazi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba, yenye lengo la kuimarisha mahusiano ya kiuchumi, uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na Qatar.

Mara baada ya kuwasili, Mhe. Kapinga alifanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Qatar, ambapo walijadili fursa za uwekezaji, biashara na masoko, pamoja na mikakati ya kuitangaza Tanzania kama eneo salama na lenye fursa kwa wawekezaji wa Qatar.

Katika ziara hiyo, Mhe. Kapinga anawakilisha sekta ya Viwanda na Biashara kwa kuendeleza juhudi za kunadi fursa za uwekezaji katika sekta za uzalishaji, viwanda, biashara na kuongeza thamani ya bidhaa, sambamba na kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi katika kukuza biashara na uwekezaji kati ya nchi hizi mbili.

Mhe. Kapinga ameambatana na viongozi na wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, akiwemo Naibu Katibu Mkuu, Aristides Mbwasi, Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE, pamoja na wataalam waandamizi.