Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Watumishi wa Wizara Watumishi waaswa kufanya kazi kwa bidii, weledi, uadilifu, uaminifu, ubunifu na upendo


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewasisitiza Watumishi wa Wizara yake kufanya kazi kwa bidii, weledi, uadilifu, uaminifu, ubunifu na upendo katika utendaji kazi wao wa kila siku ili kutimiza malengo ya Wizara na Taifa kwa ujumla katika kukuza sekta ya viwanda na biashara.

Waziri Jafo ameyasema hayo Machi 10, 2025 wakati alipokuwa akiongea na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi pamoja na kuzindua Mkataba wa Huduma kwa Wateja wa Wizara hiyo jijini Dodoma.

Katika Hatua nyingine Waziri Jafo amewapongeza Watumishi wa Wizara hiyo kwa kufanya kazi kwa bidii katika utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2024/25 na kuwaasa kuongeza bidii na ubunifu katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2025/26 hususani katika kuwezesha uanzishaji na uendelezaji wa viwanda nchini.

Naye Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe Exaud Kigahe akiongea na Wajumbe hao amewasisitiza kutekeleza Mkataba wa Huduma kwa wateja kikamilifu ili kulinda taswira ya Wizara.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Hashil Abdallah ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza hilo amesema Wizara itaendelea kuweka mazingira mazuri ya utendaji kazi ili watumishi hao waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu

Naye Katibu wa Wanawake Tughe Mkoa wa Dodoma Bi Redempta Kissima akimwakilisha Naibu Katibu Mkuu Tughe Taifa ameipongeza Wizara hiyo kwa kuwawezesha watumishi kufanya kazi vizuri, kushiriki kwenye matukio mbalimbali ya kitaifa ikiwemo siku ya wanawake duniani.

Aidha Bi Kissima amewashauri Watumishi hao kujiunga na Chama hicho cha Tughe ili kuongeza ushirikiano na kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza sehemu ya kazi.