Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Wizara ya Viwanda na Biashara yapongezwa kwa utekelezaji mzuri wa baheti ya Mwaka 2024/2025


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara,Kilimo na Mifugo chini ya Mwenyekiti wake Mhe.Deodatus Mwanyika imeipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara kwa utekelezaji mzuri wa baheti ya Mwaka 2024/2025 huku ikifurahishwa na utendaji mzuri wa Mhe. Dkt.Selemani Jafo na timu yake ya viongozi na watumishi kwa kuleta mabadiliko makubwa ya kiutendaji na kuendelea kuwa na umoja.

Kamati hiyo iliyo chini ya Mwenyekiti, Mhe. Deodatus Mwanyika imefikia hatua hiyo baada ya wasilisho la Mhe. Dkt. Selemani Jafo kuhusu taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2024/2024 na mwelekeo wa bajeti ya Mwaka 2025/2026 katika kikao cha Kamati hiyo na Watendaji wa Vizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo Machi 12,2024 Bungeni Dodoma.

Aidha, Kamati hiyo imeridhia kupitisha randama ya bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka 2025/2026 baada ya kupitia vifungu na kujiridhisha pasi shaka kuwa vinashabihiana na mapendekezo hayo.

Randama ya bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026 inalenga kutekeleza miradi mbalimbali ya Wizara ikiwa ni pamoja na kukuza Sekta za Viwanda na Biashara.