Habari
Mkutano wa nne (4) wa Kamati ya Kiufundi ya Biashara, Utalii, Viwanda na Madini ya Umoja wa Afrika

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil T. Abdallah ameongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa nne (4) wa Kamati ya Kiufundi ya Biashara, Utalii, Viwanda na Madini ya Umoja wa Afrika katika Ngazi ya Makatibu Wakuu (Tarehe 13 – 15 Mei, 2024). Aidha, Ngazi ya Mawaziri itakuwa tarehe 16 na 17 Mei, 2024.
Mkutano huu ulioanza Mei 14, 2024 unalenga kujadili masuala ya kukuza Sekta za Biashara, Utalii, Viwanda na Madini kwa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika. Mkutano husika unafanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Sipopo, Jijini Malabo - Guinea ya Ikweta