Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Mkutano wa ushirikiano kati ya Tanzania na Angola


Naibu Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe Exaud Kigahe (Mb) ameshiriki Mkutano wa pili wa Tume ya pamoja ya ushirikiano kati ya Tanzania na Angola uliofanyika Zanzibar Januari 16,2024.

Mkutano huo umeambatana na hafla ya utiaji saini wa makubaliano ya Ushirikiano (MoUs) katika sekta ya mafuta na gesi,kuondoleana visa kwa wenye hati za kusafiria za kikazi na diplomasia pamoja na sekta ya Afya.

Makubaliano hayo yamesainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb), Mhe.Ummy Mwalimu (Mb) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola Mhe. Balozi Téte Antonio.