Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Mradi wa Kuimarisha Uzalishaji Viwandani kutekelezwa Tanzania Bara na Visiwani


Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Bw. Ali Khamis Juma  ametoa rai kwa wajasiliamali na wanafunzi kutumia ipasavyo fursa ya mafunzo ya kuzalisha bidhaa zenye ubora na mbinu za kutafuta masoko yanayotolewa na BDS - KAIZEN.

Ameyasema hayo Novemba 14, 2023 alipokuwa akifungua Mkutano  wa Pamoja wa Kamati Tendaji ya utekekelezaji wa  Mradi wa Kuimarisha  Viwanda vya Uzalishaji kupitia Programu za  Huduma za Maendeleo ya Biashara  (BDS) na Uboreshaji wa Ubora na Tija (KAIZEN) uliofanyika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE),Dar es Salaam.

Amesema Mradi huo unaotekelezwa Tanzania Bara na Visiwani unalenga   kuwajengea uwezo Watanzania hususani wajasiliamali katika kuimarisha uzalishaji viwandani na mbinu za utafutaji wa masoko.

Vilevile Amesema Mradi huo pia unalenga kuwajengea uwezo  wajasiliamali kuzalisha  bidhaa zenye viwango zitakazoweza kuhimili ushindani katika soko la ndani na nje ya nchi pamoja na kukuza biashara na uchumi wa Taifa kwa ujumla.

Tanzania inatekeleza Mradi huu Awamu ya tatu kupitia Programu ya KAIZEN chini ya Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) kuanzia 2023 hadi 2027 ukilenga kutoa huduma za kibiashara kwenye sekta mbalimbali kupitia Taasisi za Serikali, Sekta  binafsi, Taasisi  za elimu

Awamu ya kwanza ya utekelezaji wa Mradi huu ilikiwa 2013 - 2017 na Awamu ya pili ilikiwa 2017 -  2021 ikilenga kuongeza tija na ubora kwenye viwanda  na  uzalishaji wa bidhaa kwa gharama ndogo nchini.