Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Mradi wa Magadisoda wa Engaruka kulisha viwanda vya vioo nchini


Waziri wa Viwanda na Biashara Dk.Ashatu Kijaji, amesema uamuzi wa Serikali wa kulipa fidia wananchi wanaozunguka mradi wa magadisoda wa Engaruka uliopo Wilaya ya Mondale mkoani Arusha.

Ameyasema hayo Mei 9, 2024 wakati wa uzinduzi wa Kiwanda kinachounganisha magari ya SINOTRUCK aina ya Howo na Tipper kilichopo Kigamboni mkoani Dar es Salaam uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema malighafi hizo zitakazopatikana katika mradi huo zitatosheleza kwa zaidi ya asilimia 99 ya mahitaji ya viwanda vya vioo hapa nchini.

" Mradi huu ni muhimu kwa uchumi wa viwanda vya vioo na kwamba hakitakiwa na haja ya kuagiza malighafi nje ya nchi,"amesema Dkt. Kijaji.

Amesema hatua hiyo ya Serikali ni ushindi mkubwa kwa uwekezaji na uzalishaji wa bidhaa za vioo hasa viwanda vilivyopo nchini.