Habari
Mwaka 2025 kipaumbele kikubwa ni pamoja na kuzindua mpango wa Miaka mitano kuanzia mwaka 2025 hadi 2030 wa ujenzi wa viwanda .

aziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Selemani Jafo(Mb) amesema katika mwaka 2025 kipaumbele kikubwa ni pamoja na kuzindua mpango wa Miaka mitano kuanzia mwaka 2025 hadi 2030 wa ujenzi wa viwanda 9,048.
Mpango huu ndani ya miaka mitano utakwenda katika mikoa na mamlaka ya serikali za mitaa, lengo kuajiri watu milioni 6.5 ambao ni wastani wa watu zaidi ya milioni moja kwa mwaka.
Amebainisha hayo Januari 03,2024 jijini Dar es Salaam akihojiwa katika kipindi cha Morning Show cha Crown Tv na kusema kupitia mpango huo utakwenda kutatua changamoto ya ajira, upatikanaji wa malighafi na kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa zinaongeza thamani nchini.
Aidha Dktl. Jafo amesema biashara ni uti wa mgongo wa taifa hivyo mwaka 2024 ulikuwa wa mafanikio zaidi kwani Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara iliweza kuzindua sera ya biashara ya mwaka 2023, kuwa na mikakati ya pamoja ya jinsi ya ushiriki wa uchumi wa taifa pamoja na kuhamasisha wawekezaji kujiingiza zaidi katika suala la viwanda ili kutoa ajira kwani Serikali pekee haiwezi kuajiri vijana wote wanaomaliza vyuo na si Serikali ya Tanzania tu hata nyinginezo duniani , hivyo ni lazima kuwa na sehemu nyingine mbadala ya kupata ajira hasa sekta binafsi kupitia viwanda.
Dkt.Jafo pia amesema Serikali ya Tanzania kwa mara ya kwanza ilisaini mkataba wa uwekezaji Maganga Matitu wa uzalishaji wa chuma ambapo ni jambo kubwa sana kwani litafanya kupiga hatua kwa sababu Tanzania inafanya uzalishaji wa chuma lakini viwanda vya chuma vina changamoto mbalimbali za kimiundombinu.
Vilevile Dkt.Jafo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ulipaji fidia ya sh. bilioni 15 katilka mradi wa Liganga na Mchuchuma baada ya kufanya tathmini, pia amesema Serikali itatengeneza kiwanda cha msingi cha utengenezaji wa magadi soda ambayo ni malighafi ya viwanda vingi.
Dkt.Jafo pia amewataka Watanzania kujua umuhimu wa kutumia bidhaa za ndani kuwawezesha vijana kupata ajira na kustawisha viwanda nchini na kuchangamkia soko huru la Afrika kwa zaidi ya