Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe ( Mb)
amefurahishwa na utendaji kazi wa Wafanayakazi katika mpaka wa Rusumo.
Mhe. Kigahe ameyasema hayo Septemba 15, 2024 alipofanya ziara ya kutemebelea mpaka wa Tanzania na Rwanda ( Rusumo ) kwa lengo kukagua na kujionea jinsi shughuli za Biashara zinazofanyika katika mpaka huo.
Akiongea wakati wa kujibu taarifa ya utendaji wa kituo hicho kutoka kwa Meneja wa kituo hicho, Mhe. Kigahe amefurahishwa na utendaji wa kituo hicho kwa uchapakazi, uadilifu na kujituma kwa watumishi.
"Nimefurahishwa na taarifa ya kutumia muda machache wa kuvusha magari na watu kwa kutumia dk 32 tofauti na upande wa pili wanaotumia muda mwingi" ,Amesema Kigahe.
Aidha, Mhe. Kigahe amesisitiza kuwa soko la Kimkakati la Kahaza linalojengwa litakapoanza kutumika lisaidie wakulima kukusanya mazao toka shambani na kuweka lebo kwenye vufungashio ili kuipa thamani bidhaa yetu kutambulika Kitaifa na Kimataifa.