Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe amesema kuwa dhamira ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sio kufanya biashara bali kuendelea kuweka mazingira rafiki


Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe amesema kuwa dhamira ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sio kufanya biashara bali kuendelea kuweka mazingira rafiki na wezeshi kwa Wawekezaji na wafanyabiashara ndani na nje ya Taifa la Tanzania.

Mhe.Kigahe amesema hayo Novemba 14,2023 alipotembelea na kuona ujenzi na uzalishaji wa kiwanda cha mbolea cha Itracom Company Limited kilichopo Nala jijini Dodoma.

Mhe.Kigahe amesema kuwa Serikali inahakikisha inaweka mazingira rafiki kwa sektaa binafsi kwani ndio zenye mchango mkubwa katika ujenzi wa viwanda Nchini na uwepo wa Kiwanda hicho cha Itracom ni matokeo chanya ya jitihada za Serikali za kuhakikisha mazingira bora ya ufanyaji biashara Nchini.

Aidha Mheshimiwa Naibu Waziri amekipongeza kiwanda hicho kwa kuhakikisha kinazalisha na kusambaza mbolea ndani ya nchi kwa ruzuku ya Serikali lakini pia kwa kuwa kiwanda kinachozalisha na kusambaza mbolea nje ya mipaka ya Tanzania.

Vilevile mhe.Kigahe amewataka wafanyakazi wa Kiwanda hicho kuwa mstari wa mbele katika kukisemea vyema Kiwanda hicho pamoja na kufanya kazi kwa bidii ili kujenga ufanisi lakini wakati huohuo ameuataka uongozi wa Kiwanda hicho pia kusimamia maslahi ya Wafanyakazi wake kama sharia za Nchi zinavyotaka.

Akizungumza Kwaniaba ya Mwenyekiti wa bodi ya Kiwanda hicho Ndg.William Ngeleja ameishukuru Serikali kwa kukubali na kuridhia kutoa nafuu ya baadhi ya Changamoto katika kipindi cha uwekezaji wa kiwanda hicho.

Naye Mkurugenzi wa Kiwanda hicho Ndg.Nazaire Nduwimana amesema kuwa Kiwanda kitakaokamilika kitakuwa na uwezo wa kutoa ajira 2000 mpaka 3000 na mpaka sasa Kiwanda hicho kinazalisha mbolea za aina 4 ambazo ni mbolea ya kuotesha,kuneneesha,kukuzia na mbolea maalum kwa mazao ya biashara.