Habari
Upatikanaji wa Vifaa bora vya Maabara vitarahisisha utendaji kazi katika Shirika la Viwango Tanzania (Tbs).
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Wizara ya Viwanda na Biashara Bw.Sempeho Nyari Manongi amesema kuwa upatikanaji wa Vifaa bora vya Maabara vitarahisisha utendaji kazi katika Shirika la Viwango Tanzania (Tbs).
Ndg.Sempeho amebainisha hayo akimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Selemani Jafo(Mb) katika hafla ya kupokea Vifaa vya Maabara kutoka Umoja wa Ulaya (EU) vilivyokabidhiwa kwa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kupitia mradi wa QUALITAN leo Juni 18,2025 katika Ofisi za Shirika hilo Jijini Dar es Salaam.
Bw.Sempeho amesema vifaa hivyo vitarahisisha upimaji wa sampuri kwa muda mfupi hivyo wajasiriamali na wafanyabiashara nchini wamehakikishiwa kuwa upimaji wa sampuri na bidhaa zao zitapimwa kwa ufanisi na uharaka zaidi ili kurahisisha biashara ndani ya nchi pamoja na nje ya nchi wanapotaka kusafirisha bidhaa zikiwa na viwango bora.
Aidha Bw.Sempeho amesema vifaa hivyo vitaongeza uwezo zaidi katika kuhakikisha bidhaa za Tanzania kuingia katika masoko ya nje,hivyo wajasiriamali na wafanyabiashara watumie fursa hiyo kupitia (TBS) kuingia sokoni.
Kwa upande wa Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Balozi Christine Grau amesema kutoa vifaa hivyo vya kisasa kwa TBS ni harakati za umoja hho kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania kuboresha ubora na ushindani wa bidhaa zinazozalishwa nchini ili ziweze kuingia Kwa urahisi zaidi kwenye masoko ya kimataifa.
Nae Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Dkt.Ashura Katunzi amesema kuwa licha ya ununuzi wa vifaa hivyo pia mradi umeweza khijengda uwezo taasisi katika masuala ya kidijitali,miundombinu na Mifumo na mafunzo ya kitaaluma.