Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Siku ya wanawake Duniani kuwatembelea wahitaji waliopo katika Gereza la Isanga mkoani Dodoma.


 

 

Watumishi (Wanawake) wa Wizara ya Viwanda na Biashara wameazimisha siku ya Wanawake ya Kimataifa Machi 8, 2025 kwa kufanya tendo la huruma kwa kuwatembelea wahitaji waliopo katika Gereza la Isanga mkoani Dodoma.

Ujumbe huo wa Wanawake umeongozwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Utumishi na Utawala wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Bi. Veronica Nchango na kupokelewa na Mkuu wa Gereza la Isanga, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza( ACP), Zephania Neligwa pamoja na msaidizi wake sehemu ya Gereza la wanawake Afande Kilambo.