Habari
ZAIDI YA WASHIRIKI 300 WAMEJIANDIKISHA KUSHIRIKI MAONESHO YA EXPO 2025 JAPAN.
ZAIDI YA WASHIRIKI 300 WAMEJIANDIKISHA KUSHIRIKI MAONESHO YA EXPO 2025 JAPAN.
Waziri wa Viwanda na Biashara (mb) Dkt. Selemani Jafo amesema mpaka sasa Washiriki zaidi ya 300 kutoka Tanzania wamejiandikisha kushiriki Maonesho ya Expo 2025 yatakayofanyika Nchini Japan.
Dkt.Jafo amesema kutoka Tanzania imelengwa kuwa na Washiriki zaidi ya 500 ambao watawakilisha Taifa Nchini Japan..
Aidha, ameeleza kuwa maonesho hayo yatakuwa na siku maalum kwa kila sekta, ikiwemo utalii, uchumi wa buluu, miundombinu, uchukuzi, n.k pia ameongeza kuwa Tanzania inalenga kuongeza pato la taifa GDP, kupitia fursa zitakazopatikana kwenye maonesho hayo. Kwa sasa, GDP ya Tanzania iko katika wastani wa dola za Kimarekani bilioni 80.
Waziri huyo alibainisha kuwa Siku ya Taifa ya Tanzania katika maonesho hayo itakuwa Mei 25, 2025 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania TPSF Bi.Angelina Ngalula, amesema kuwa Tanzania ilisaini mikataba yenye thamani ya zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 8 katika Expo 2024, ambapo mingine tayari imeanza kutekelezwa, ikiwemo uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam.
Vilevile ametoa wito kwa wafanyabiashara wanaotaka kushiriki kuhakikisha wanapeleka taarifa mapema na kuwa na mipango ya biashara ‘business plan’ iliyoandaliwa vizuri, ili kuwasaidia kupata washirika wa kibiashara.
Pia, fursa nyingine zilizotajwa ni pamoja na sanaa na utamaduni, ambapo Angelina alisema watu wengi nchini Japan wanapenda muziki wa Tanzania na filamu za ‘Bongo Movie hivyo Wasanii kuweza kutumia maonesho hayo kama jukwaa la kuonesha kazi zao kimataifa.