Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

KATIBU MKUU WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA AKAGUA MAANDALIZI YA UZINDUZI WA SERA DODOMA


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Balozi Waziri Rajab Salum, leo Oktoba 31, 2026, ameongoza Kamati ya Maandalizi ya uzinduzi wa Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda ya Mwaka 2025 na Sera ya Maendeleo ya Wajasiriamali Ndogo na wa Kati (Toleo la 2025), kutembelea Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma kwa ajili ya kukagua maandalizi ya uzinduzi wa sera hizo.

Sera hizo zinalenga kuimarisha maendeleo ya viwanda na ujasiriamali nchini kwa kuongeza uzalishaji, ajira, thamani ya malighafi za ndani, upatikanaji wa mitaji na masoko kwa wajasiriamali, huku Serikali ikilenga kuongeza mchango wa sekta ya viwanda hadi kufikia asilimia 15 ya Pato la Taifa.

Kuelekea uzinduzi huo, Novemba 2, 2026, kutakuwa na maonesho na kliniki za biashara, yakifuatiwa na kongamano la wadau wa Viwanda na Biashara Novemba 3, kabla ya uzinduzi rasmi wa sera hizo Novemba 4, 2026, katika ukumbi wa mikutano Jakaya Kikwete Convention Centre, jijini Dodoma. ambapo Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi.