Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

WAZIRI MKUU AIAGIZA TANTRADE KUFANYA TAFITI YA MASOKO NDANI NA NJE YA NCHI.


WAZIRI MKUU AIAGIZA TANTRADE KUFANYA TAFITI YA MASOKO NDANI NA NJE YA NCHI.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa ameiagiza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kuendeleza juhudi za kutafuta masoko ya nje ili kuongeza mauzo yatakayowezesha nchi kupata fedha za Kigeni.

Ametoa agizo hilo alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufungaji wa Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar-es-Salaam Julai 13, 2025

Amesema kuwa TanTrade inapaswa kufanya tafiti za uhakika na uchambuzi wa masoko ambayo bidhaa za Tanzania zinaweza kuuzwa na kutoa taarifa hizo kwa wafanyabiashara kote nchini.

Mhe Majaliwa amesena TanTrade wanatakiwa kufanya tafiti za uhakika na uchambuzi wa kina kwani Masoko yamekuwa ya ushindani sana katika kipindi hiki kama Soko Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo katika kufanya uchambuzi wa masokot, hayo ndio maeneo ya kufanya biashara,

Aidha, Mhe. Majaliwa ametoa wito kwa wazalishaji wote nchini kuweka mkakati wa kuongeza uwekezaji na uzalishaji wa bidhaa zenye ubora ambazo zina mahitaji makubwa katika masoko ndani na nje ya nchi kwa kupata mwanga kupitia maonesho kwa kujua bidhaa gani zina mahitaji makubwa ili kuongeza uzalishaji kwa kupanua wigo wa masoko kwenye mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi.

Pia Mhe. Majaliwa amezitaka taasisi zote zinazosimamia Biashara na Uwekezaji, Tanzania Bara na Zanzibar, zihakikishe zinaondoa urasimu na kuwezesha Biashara zaidi badala ya kuwa kikwazo.

Kwa Upande wake, Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo katika kipindi cha siku 16 cha maonesho hayo, watu zaidi ya milioni 2.4 wameweza kushiriki katika shughuli mbalimbali za maonesho hayo ya kimaitaifa ya biashara.

Pia ameongeza kuwa kupitia nembo ya Made in Tanzania, itaiwezesha nchi kuuza biadhaa zikiwa na nembo ya Taifa Kwani fahari kubwa sana Watanzania.