Habari
Taarifa ya Wizara ya Viwanda na Biashara ya utekelezaji wa Maazimio kuhusu kanuni za nidhamu kwa wanafunzi wa CBE 2024
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo imepokea na kiridhia Taarifa ya Wizara ya Viwanda na Biashara ya utekelezaji wa Maazimio kuhusu kanuni za nidhamu kwa wanafunzi wa CBE 2024 na utekelezaji wa uchambuzi wa sheria ndogo kuhusu Kanuni za uongezaji wa virutubishi kwenye chakula TBS 2024
Kamati hiyo ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake Mhe. Ramadhan Suleiman imepokea na kiridhia Taarifa hiyo iliyowaailishwa na Wizara ya Viwanda na Biaahara Machi 28, 2025 Bungeni jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Exaud Kigahe akiwa ameambatana na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Needpeace Wambura , Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Prof. Edda Lwoga pamoja na Viongozi wengine wa Wizara , CBE na TBS aliwasilisha Taarifa hiyo na kuiahidi Kamati hiyo kutekeleza kikamilifu sheria ndogo na kanuni zilizorid