Habari
Semina kuhusu malengo na nia njema ya Serikali ya awamu ya Tano kuhamishia makao ya nchi Mkoani Dodoma.
Wafanyakazi wa wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji wapewa semina kuhusu malengo na nia njema ya Serikali ya awamu ya Tano kuhamishia makao ya nchi Mkoani Dodoma. Semina hii imeendeshwa na Kaimu kamishina wa Ustawi wa Jamii ndugu. Rabikira O. Mushi, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Ndugu. Patrick, Afisa Ustawi wa Jamii mwandamizi ndugu. Darius Kalijongo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ndugu. Tutubi Mangazeni. Semina hii imelenga zaidi kujadili fursa mbalimbali zilizoko katika Mkoa huo na pia kujiandaa kisaikolojia kuhamishia makazi Dodoma ambako ndio Makao makuu ya nchi ili kuwahudumia watanzania kwa karibu zaidi.