Habari
Serikali imeweka uwekezaji mkubwa katika sekta ya kilimo hivyo ni vema kuongeza zaidi uzalishaji na masoko ili kukuza biashara.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Suleiman Jafo amesiaitiza kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika sekta ya biashara ikiwemo kushughulikia changamoto za kikodi na kutoa fursa kwa Tanzania kukua kwa kibiashara
Waziri Jafo ameyasema hayo Novemba 29, 2024 wakati akiongea na vyombo vya habari kabla ya Mkutano wa 24 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Arusha tarehe 29 na 30 Novemba 2024.
Alisema Serikali imeweka uwekezaji mkubwa katika sekta ya kilimo hivyo ni vema kuongeza zaidi uzalishaji na masoko ili kukuza biashara.
Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi mahamoud Thabit Kombo alitoa rai kwa watanzania kujiandaa zaidi katika masoko ikiwemo kuuza kwa nchi za EAC na Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC) hivyo lazima barabara ziongezwe,treni ya SGR kukamilishwa zikiwemo bandari ili kuhakikisha watanzania wanajitayarisha kujikwamua kiuchumi kupitia sekta ya miundombinu ikiwemo bandari na uongezaji wa vyombo vya usafiri.