Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya wafanyabiashara


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah amesema Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya wafanyabiashara ili watimize ndoto na maono waliokusudia kwa kuwanufaisha zaidi Watanzania.

Dkt.Abdallah ameyasema hayo Septemba 7, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Dkt. Selemani Jafo (Mb) kwenye sherehe ya miaka 20 ya Kampuni ya Dar es Salaam Corrido Group Co.Ltd.