Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Serikali inaendelea kufanya kila linalowezekana kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha zoezi la uokoaji linafanyika kwa haraka na ufanisi mkubwa.


waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt. Selemani Jafo (Mb) amesema Serikali inaendelea kufanya kila linalowezekana kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha zoezi la uokoaji linafanyika kwa haraka na ufanisi mkubwa.

Ameyasema hayo alipofika Kariakoo kuona zoezi la uokoaji kufuatia kuanguka kwa ghorofa
la Biashara Kariakoo Novemba 16,2024 Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Jafo ametoa rai kwa Wananchi kuendelea kuwa na subira wakati shughuli za uokoaji zinaendelea na imani yake kuwa uokoaji utaenda vizuri na kwa ufanisi mkubwa.

Aidha Dkt.Jafo ametoa salamu za pole kwa familia mbalimbali zilizopoteza wapendwa wao ,Majeruhi na Wafanyabiashara kwa ujumla kufuatia ajali hiyo.

Vile vile amevipongeza vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama,Taasisi pamoja na Wananchi kwa ushirikiano wao wa kuendelea kuokoa majeruhi wa ajali hiyo.