Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki ya biashara ili kuwezesha upatikanaji wa ajira kwa watanzania.


Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewahakikishia wafanyabiashara kuwa Serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki ya biashara ili kuwezesha upatikanaji wa ajira kwa watanzania.

Hayo yalisemwa Januari 9, 2025 Jijini Arusha wakati wa ziara ya kutembelea kiwanda cha magodoro cha Tanfoam kwaaajili ya kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji zinazofanyika na kusikiliza changamoto za kibiashara..

Dkt.Jafo alisema serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki ya biashara yenye lengo la ukuzaji uchumi na wananchi kupata ajira hususan vijana na wanawake sanjari na kuhakikisha wafanyakazi wanapata stahiki zao

Pia alikipongeza kiwanda cha Tanfoam kwa kuendelea na ujenzi wa kiwanda kipya eneo la Moshono Jijini Arusha ambapo kiwanda hicho licha ya ufinyu wa eneo lakini kinaendelea na shughuli za uzalishaji katika eneo la Ungalimited ambacho kinatarajia kuongeza ajira kutoka 400 hadi kufikia ajira 700.

"Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki ya biashara sanjari na ukuzaji wa uchumi ikiwemo utatuzi wa changamoto mbalimbali kwa wawekezaji lengo kukuza ajira kwa watanzania"

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Kiwanda cha TANFOAM,Meshack Jimy alisema upanuzi wa kiwanda hicho eneo la Moshono utaongeza ajira kwa watanzania sanjari na ongezeko la mitambo kwani kampuni hiyo kwa hivi sasa inaendesha kiwanda katika hali ya ufinyu wa eneo lakini ujenzi wa kiwanda kipya hadi kukamilika kwake kutawezesha mitambo mipya na mingineyo kusimikwa ili kuongeza uzalishaji zaidi

Alisema pia wataongeza mitambo mingine ya uzalishaji wa bidhaa zao na kuishukuru serikali kwa kuweka mazingira mazuri ya ufanyaji kazi na kuongeza uzalishaji ikiwemo ulipaji wa kodi.

Wakati huo huo, Frank Mbando ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulika na usimamizi wa shughuli za Viwanda na Biashara Mkoani Arusha alisema ziara ya Waziri Dk, Jafo inatoa hamasa katika sekta ya viwanda katika uwekezaji ikiwemo utatuzi wa changamoto zinazowakabili wenye viwanda na kuajiri watanzania zaidi ya 300.

Alisema kiwanda hicho kinazalisha magodoro yenye viwango bora ndani na nje ya nchi na inazalisha magodoro pisi 14,000 kwa mwezi na kusisitiza pia kiwanda hicho kitakapokamilika kitaongeza