Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt Selemani Jafo (Mb), amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira bora ya ufanyaji biashara ikiwemo kuboresha miundombinu na usafiri,na TEHAMA ili kurahisisha biashara, kupunguza gharama,kukuza ubunifu kwa kuhimiza uzalishaji wa bidhaa na hudumabora ili kukidhi mahitaji yanayobadilika ya soko la ndani na njeya nchi likiwemo Soko la Marekani
Dkt. Jafo ameyasema hayo Agosti 20, 2024 wakati akifunguaMaonesho ya Maendeleo ya Mradi wa Biashara na Uwekezaji Afrika (ATI) chini ya Shirika la Misaada la Marekani (USAID)yaliyofanyika katika Hotel ya Hyatt jijini dar es Salaam.
Aidha Dkt Jafo amesema kuwa kuna haja ya kuendelea kukuzana kuimarisha uwezo wa uzalishaji na usambazaji ili kukidhimahitaji ya soko, kupanua kapu la mauzo ya nje kwa kupanuazaidi ya sekta za jadi ili kujumuisha bidhaa zilizoongezwathamani na zenye viwango vya juu.
Vilevile amebainisha kuwa Mradi USAID Afrika (ATI) umekuwa chachu katika kukuza uchumi na kuboresha maisha ya watu wa Tanzania kwa kuwawezesha wafanyabiashara na kukuza ubunifu katika sekta muhimu za uchumi ambapo kupitia Mradi huo Tanzania imeshuhudia ongezeko la mauzo ya baadhi ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi chini ya usaidizi wa ATI, uzalishaji wa ajira mpya, na uwezeshaji wa wajasiriamali ambao sasa wanachangia kuimarika kwa uchumi wa nchi
Naye Mkurugenzi Mkazi “Mission Director” wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Bw. Craig Hart amesemaSerikali ya Marekani kupitia USAID, itawekeza ruzuku ya Dola za Marekani milioni 8.3 kwa kampuni tisa za Tanzania ambazo ni BioBuu, Biotan Limited, Central Park Bees, Minjingu Mines and Fertilizer Limited, Mount Meru Millers, Red Earth Limited, Sabayi Investments Limited, Tanzania Tooku, Garments Co. Ltd na Mtu wa Tatu (Love Honey) ili kukuza biashara, kuboresha usalama wa chakula na kuiwezeshaTanzania kuongeza ushindani katika mauzo ya nje kupitiaMpango wa Ukuaji na Fursa Afrika (AGOA) na kuifanyaTanzania kuwa kikapu cha chakula kikanda, muuzaji nishatinje, na kitovu cha ubunifu unaoendeshwa na vijana.