Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Serikali kuhakikisha Taasisi zake zinazotumia bidhaa na vipuri vinavyozalishwa na KMTC


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exhaud Kigahe (Mb) amesema Mkakati wa Serikali ni kuhakikisha kuwa Taasisi zake zinazotumia bidhaa na vipuri vinavyozalishwa na KMTC zinaingia mikataba ya kununua mashine na vipuri kutoka Kilimanjaro Machine Tools

Kigahe amesema hayo Novemba 1,2023 Bungeni Dodoma wakati akijibu swali la Mhe. Saasisha Elinikyo Mafuwe kuhusu Serikali ina mkakati gani wa kuelekeza Taasisi zake kununua mashine na vipuri katika kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools?

Amesema Serikali kupitia Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) imekifanyia ukarabati mkubwa katika kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools (KMTC) ikiwa ni pamoja na kujenga tanuri la kuyeyushia chuma (Foundry), ukarabati wa miundombinu ya kiwanda na utengenzaji wa mtambo wa kuweka utando katika bidhaa za chuma ili kuzuia kutu (Hot Dip Galvanizing plant).

Aidha amesema mikakati ya Serikali nikuona rasilimali zake zinatumika kuzalisha bidhaa ambazo zinahitajika kutumiwa hasa kwenye bidhaa za Chuma nchini

Vile vile amesema utekelezaji wa Mradi wa Liganga na Mchuchuma baada yakukamilisha majadiliano na mwekezaji malighafi ya Chuma ndio itakayotumika katika viwanda nchini ikiwemo cha Kilimanjaro Machine Tools

Aidha amesema Serikali Kupitia NDC imefanya majadiliano na ishaweka mpango mkuu kwa ajili ya eneo la kibiashara katika eneo la Kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools ili kuweza kuwasadia wana Hai kwa kuangalia mahitaji mahsusi yanayopaswa kupewa katika eneo hilo