Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Serikali kuwachukulia hatua kali za Sheria wazalishaji wa bidhaa za saruji nyeupe watakaokiuka sheria, taratibu na kanuni za Biashara.


 

 

Serikali kuwachukulia hatua kali za Sheria wazalishaji wa bidhaa za saruji nyeupe watakaokiuka sheria, taratibu na kanuni za biashara.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Dkt.Selemani Jafo (Mb) alipokutana na kujadiliana na wazalishaji wa bidhaa za saruji nyeupe (wall putty) Januari 15, 2025 jijini Dodoma.

Mhe.Jafo amesema kuwa kuna baadhi ya wazalishaji wa bidhaa ya saruji nyeupe ambao wamekuwa wakiweka vitu vingine kwenye mifuko (vocha za simu, 'coupons' za zawadi nk) kwa lengo la kuwavutia wateja na kupandisha bei ya bidhaa hiyo bila kufuata sheria, taratibu na kanuni.

Aidha, wazalishaji wa bidhaa hiyo wameonywa kuacha tabia hiyo mara moja na ifikapo Februari 1, 2025 msako mkali utaendelea viwandani na sokoni.

Hatahivyo, wazalishaji wa bidhaa wameelekezwa kuhakikisha kuwa kabla ya kupeleka bidhaa zao sokoni ni sharti waanzie ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na ofisi za Wakala wa Vipimo (WMA).