Habari
Serikali kuwasaidia wakulima na wazalishaji chumvi ghafi nchini kuwa na soko la uhakika

Serikali kuwasaidia wakulima na wazalishaji chumvi ghafi nchini kuwa na soko la uhakika
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akiwa na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde (Mb) pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah wamekutana na wakulima na wazalishaji wa chumvi nchini Novemba 16, 2023 jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili changamoto za soko la chumvi ghafi nchini ili kuwasaidia kuwa na masoko ya uhakika ndani na nje ya nchi