Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Serikali Nchini kuhakikisha wanajenga mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa ndani na nje ya Nchi


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Exaud Kigahe (Mb) ameziagiza Taasisi za Serikali Nchini kuhakikisha wanajenga mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa ndani na nje ya Nchi ili waweze kuzalisha bidhaa bora zitakazohimili ushindani katika soko la Jumuia ya Afrika Mashariki na nje ya Afrika.

Naibu Waziri Kigahe ameyasema hayo katika majumuisho ya ziara yake aliyoifanya katika Kiwanda cha kuchakata Alizeti cha Bugali Investment LTD, pamoja na Kiwanda cha kuchambua Pamba cha Alliance Ginneries Februati 22, 2025 Wilayani Bariadi.

Amesema iwapo Serikali itajenga mazingira wezeshi kwa Wawekezaji wa ndani na nje ya Nchi itachochea kwa kiasi kikubwa kuimarika kwa Sekta binafsi jambo litakalosaidia kukuza Uchumi wa Nchi.

Naibu Waziri Kigahe yupo katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Simiyu kwa lengo la kutembelea Viwanda na kuzungumza na Wafanyabiashara.