Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Serikali yawakaribisha wafanyabiashara wa Saudi Arabia nchini


Serikali imewakaribisha wafanyabiashara wa Saudi Arabia kuja kufanya Biashara Tanzania katika sekta za Kilimo, Viwanda, Mifugo, Nishati, Madini, Utalii, Madawa na Miliki ya Ujenzi (Real Estate). 

Wafanyabiashara hao wamekaribishwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akiwa na ujumbe wake Aprili 29, 2024 alipokutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara na Viwanda ya Saudi Arabia, Mhe. Hassan Al-Huwaizi, wakati waMkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani unaloendelea Jijini Riyadh, Saudi Arabia.

Naye Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara na Viwanda ya Saudi Arabia, Mhe. Hassan Al-Huwaizi na ujumbe wake ameridhia kuwaunganisha wanyabiashara na wawekezaji  kutoka Saudi Arabia kuja kuwekeza Tanzania. 

Aidha, kwa upande wa Tanzania, Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Taasisi zake za WRRB na TANTRADE wameonesha uhakika wa kutoa ushirikiano mkubwa kwa kushirikiana na taasisi za sekta husika pamoja na Kituo cha Uwekezaji. 

Dkt Kijaji aliongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo uliowajumuisha  Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha Bw. Rashed Bade, Mkurugenzi wa  Idara ya Maendeleo ya  Biashara Bw. Sempeho Manongi, Mkurugenzi  Mkuu wa Bodi ya Maghala Bw. Asangye Bangu, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa  TanTrade Bw. Deo Shayo, na maafisa wa Ubalozi wa Tanzania, Saudi Arabia