Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) yasaini makubaliano ya ushirikiano na Uturuki.


Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) yasaini makubaliano ya ushirikiano na shirika la kuhimiza viwanda vidogo na kati la Uturuki. Makubaliano yamesainiwa tarehe 23 januari, 2017 ambapo wafanyabiashara kutoka Uturuki watawekeza katika Viwanda mbalimbali ili kuinua sekta hii na itakuza uchumi wa nchi. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage alisisitiza azima ya Uturuki kuongeza uwekezaji hapa nchini hadi kufikia dola 500 milioni za kimarekani.