Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

MKUTANO WA WADAU SIMANJIRO WAJADILI MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA (WRS)


Mkutano maalum wa wadau wa kilimo umefanyika katika Wilaya ya Simanjiro, ukihusisha viongozi na wataalam mbalimbali kujadili utekelezaji wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala (WRS).

Miongoni mwa washiriki walikuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Mheshimiwa Fakii Lulandala; Mkurugenzi wa Halmashauri, Bw. Gracian Makota; Kaimu Mwenyekiti wa Bodi, Bw. Alex Ndikile; Mkurugenzi Mtendaji wa WRRB, Bw. Asangye Bangu; Mrajis Msaidizi wa Manyara, Bw. Absolum Cheliga pamoja na Maafisa wa Kilimo, Biashara na Mapato.

Katika kikao hicho, wadau walikubaliana maazimio kadhaa muhimu ikiwemo:
• Ujenzi wa ghala kuu la mnada Simanjiro
• Kuongeza uhamasishaji kuhusu matumizi ya WRS
• Kuwezesha uundwaji wa vyama vya ushirika
• Kuimarisha upatikanaji wa pembejeo na mbegu bora ili kuongeza uzalishaji wa ufuta na maharage

Akizungumza katika mkutano huo, viongozi walisema kuwa utekelezaji wa maazimio hayo utasaidia wakulima kunufaika zaidi kupitia biashara yenye tija na masoko yenye uhakika.

WRRB imesisitiza itaendelea kushirikiana na wadau wote kuhakikisha wakulima wa Simanjiro na maeneo mengine wanapata manufaa ya moja kwa moja kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala