Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb.) amesema Kongamano la Tano la Maendeleo ya Biashara na Uchumi Uchumi, lililoandaliwa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Tawi la Dodoma linasaidia kuibua mijadala itakayowezesha kubaini changamoto na fursa zitazoisaidia nchi kupata mafanikio katika sekta ya biashara na uchumi ikiwemo kuongeza ajira.
Ameyasema hayo Novemba 22,2024 wakati akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufungua Kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma
“Takwimu za mwaka 2001 vijana waliomaliza vyuo vikuu, walikuwa 51800, na kadiri miaka inavyoenda ndivyo wanavyoongezeka, Serikali pekee haiwezi kuajiri, tunategemea wengine waende sekta binafsi, tunazo fursa za masoko kwenye nchi za SADC, Afrika Mashariki, na la huru za afrika; ili kuweza kuyafikia masoko hayo lazima tufanye tafiti”. Alibainisha Dkt. Jafo.