Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Tanzania inazo fursa nyingi na mazingira salama kwa Wawekezaji na Wafanyabiashara kutoka nchini India,


Naibu Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe (Mb) amesema kuwa Tanzania inazo fursa nyingi na mazingira salama kwa Wawekezaji na Wafanyabiashara kutoka nchini India, ambao wengi wao wameanzisha Viwanda na wengine wanafanya biashara na kutengeneza ajira kwa Watanzania.

Amebainisha hayo katika Ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji na Biashara baina ya Tanzania na Ujumbe wa Wawekezaji na wafanyabiashara kutoka nchini India linalofanyika Julai 15, 2025 katika Ukumbi wa JNICC, jijini Dar es Salaam.

Mhe.Kigahe amesema kuwa kuwepo kwa malighafi, nguvu kazi, wanunuzi wa bidhaa na mazingira rafiki ya Kibiashara kutasaidia wawekezaji kupata faida na kuwavutia wengine kuja kuwekeza Tanzania.

Aidha, Mhe.Kigahe ametoa rai kwa Wafanyabiashara na wawekezaji nchini Tanzania kuendelea kutumia nembo ya 'Made in Tanzania' ili bidhaa zote ziweze kutambulika kirahisi zaidi katika masoko ya ndani na nje ya nchi ili kupata masoko ya bidhaa zaidi.

Naye Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Kapufi Mbega amesema kuwa Wahindi wapo vizuri katika umiaji wa mbogamboga na matunda. Hivyo amewashauri kuja kuwekeza katika kilimo, utamaduni wa lugha na mtindo wa maisha.