Habari
Tanzania imepiga hatua kuzalisha na kusambaza umeme vijijini

Waziri wa Viwanda na Biashara,Mhe Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amesisitiza kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuzalisha na kusambaza umeme vijijini na mjini.
Waziri kijaji ameyasema hayo Aprili 29, 2024 alipokuwa akishiriki Mjadala kuhusu mageuzi ya nishati duniani wakati waMkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani unaloendelea Jijini Riyadh, Saudi Arabia.
Vilevile ametoa wito kwa nchi zilizoendelea kiviwanda kuunga mkono juhudi hizo ili kuimarisha uzalishaji viwandani.
Dkt kijaji anaongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo unaowajuisha Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara Bw. Sempeho Manongi, Mkurugenzi wa Bodi ya Maghala Bw. Asangye Bangu, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bw. Deo Shayo, Kamishna wa Fedha za Nje Bw. Rashed Bade na Maafisa Waandamizi wa Ubalozi wa Tanzania- Riyadh Saudi Arabia.