Habari
Tanzania imeweka mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji ikiwemo mifumo ya Sera, Sheria na Uratibu ili kukuza biashara na kuvutia wawekezaji

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji ikiwemo mifumo ya Sera, Sheria na Uratibu ili kukuza biashara na kuvutia wawekezaji
Aidha Kijaji ameshauri umuhimu wa Mpango wakuongezwa kwa muda mrefu zaidi kuanzia miaka 20 ili uweze kuvutia wawekezaji wakubwa wa ndani na nje ya nchi.
Dkt Kijaji ameyasema hayo Novemba 2, 2023 alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Watumishi wa Mshauri Mkuu wa Biashara, katika Kamati ya Mipango (Ways and Means) ya Baraza la Wawakilishi (House of Representatives) ya Marekani Bw. Alexandra Whittaker wakati wa Kongamano la 20 la AGOA Johannesburg, Afrika Kusini
Akizungunza Bw. Whittaker allyeongozana na ujumbe wa Watumishi Saba (7) kutoka Kamati ya Mipango (Means and Ways) ya Bunge la Wawakilishi na Kamati ya Fedha ya Bunge la Senati ambao waliwawakilisha Wawakilishi (Representatives) wa Kamati hizo. Aliujulisha ujunbe huo umuhimu wa AGOA kwa Tanzania na nchi nyingine za Afrika kwenye uchumi na ajira hususan za Wanawake na Vijana.
Bw. Whittaker amesema kuwa vyama vyote vya Democratic and Republic vinaunga mkono suala la AGOA. Na ameshauri kuhusu matumizi ya miundombinu za kidigitali (digital infrastructure), kuongeza uzalishaji wa nishati mbadala na uongezaji thamani kwenye madini muhimu kama vile lithium.
Vile vile Bw. Whittaker amesema kamati hiyo huwa ina majukumu kubwa lakutafuta vyanzo vya fedha kwa ajili ya kuendesha shughuli za Serikali ya Marekani