Habari
Tanzania ipo tayari kuhakikisha mazingira ya ufanyaji biashara yanaendelea kuboreshwa na kuwa wezeshi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil T. Abdallah amesema Tanzania ipo tayari kuhakikisha mazingira ya ufanyaji biashara yanaendelea kuboreshwa na kuwa wezeshi kwa kuzingatia ubora wa bidhaa kwa walaji
Dkt Abdallah ameyasema hayo Septemba 04, 2024 wakati akimuakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara kwenye Jukwaa la Mfumo wa Chakula Afrika (Africa Food System Forum) linalofanyika kwenye Kituo cha Mikutano Kigali, Rwanda.
Amefafanua kuwa Tanzania inandelea kichukua hatua mbalimbali katika kuboresha mazingira hayo ya biashara kwa kutekeleza Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara Nchini (MKUMBI) ikiwemo kurekebisha Sera na Sheria mbalimbali zinazohusu ufanyaji biashara, Miundombinu ya Barabara, Reli ya Kisasa na Umeme.
Sambamba na Jukwaa hilo linaloongozwa na kauli mbiu isemayo Innovate, Accelerate and Scale: Delivering food systems transformation in a digital and climate era” Dkt Abdallah amesema
Tanzania inafanya Mikutano ya Uwili kuhusu Mfumo Rahisi wa Ufanyaji Biashara Mipakani (STR) na Nchi za Malawi na Msumbiji.
Jukwaa la AFS (ambalo hapo awali lilijulikana kama AGRF limehudhuliwa na Maafisa wa Serikali, Watunga Sera, Wanazuoni, Wajasiriamali, Wakulima na Asasi za Kiraia kwa ajili ya kujadili maendeleo, kubadilishana uzoefu, na kuangazia sera na mifumo mbalimbali, uvumbuzi wa teknolojia, mbinu bora, masuala ya biashara, na fursa za uwekezaji zenye uwezo mkubwa wa kuharakisha mabadiliko ya mifumo ya chakula barani Afrik