Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Tanzania kushiriki Mkutano wa tano wa Kimataifa wa maandalizi ya Expo 2025


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt Hashil Abdallah ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano wa tano wa Kimataifa wa maandalizi ya Expo 2025 utakaofanyika Osaka nchini Japan kuanzia tarehe 13 Aprili-13 Oktoba, 2025.

Mkutano huo umeanza leo Januari 15-16, 2025 ambapo Dkt. Abdallah ameambatana na Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade @tantradetz Bi. Latifa Khamis na Wataalam kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara na Wizara ya Mambo ya Nje, Ubalozi wa Tanzania nchini Japan na TanTrade.