Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Tanzania yazindua mkakakati wa kitaifa wa AFCFTA


Tanzania yazindua mkakakati wa kitaifa wa AFCFTA

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Selemani Jafo amesema Tanzania ina kila sababu ya kuongeza uwezo wa uzalishaji wa bidhaa bora na shindani kwa ajili ya kuuza katika nchi za Afrika chini ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AFCFTA) hatua itakayosaidia kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi

Ameyaeleza hayo Julai 24,2025 jijini Dar es salaam wakati akizindua Mkakati wa miaka 10 wa kitaifa wa utekelezaji wa mkataba wa AFCFTA

Aidha amesema Mkakati huo unalenga kuharakisha utekelezaji wa Mkataba wa AfCFTA nchini Tanzania, kwa kuunganisha sera na mifumo iliyopo ili kubaini fursa za kuongeza thamani, biashara, kukabiliana na vikwazo visivyo vya kiushuru, na kuimarisha uwezo wa sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika soko hilo linalokadiriwa kuwa na watu bilioni 1.

Naye Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana , Ajira , Kazi na Watu wenye Ulemavu Mhe. Ridhwan Kikwete amesema Baadhi ya wafanyabiashara wanaofanya bishara Africa chini ya AFCFTA wanasema Mkataba huo umekuja wakati sahihi ambapo takribani kampuni 43 zimeanza kuuza bidhaa Afrika chini ya AfCFTA

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi amesema Mhe. David kihenzile amesema miundombinu ya usafirishaji wa bidhaa kwenda katika masoko ya Afrika na fursa za ajira inawekwa bayana ili kusaidia nchi kunufaika zaidi na AfCFTA.

Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA) ni mpango kabambe wa Umoja wa Afrika (AU) uliosainiwa na nchi 54 kati ya 55 wanachama wa AU ukilenga kuunda soko la pamoja lenye watu bilioni 1.4 barani kote kwa kuondoa ushuru wa forodha na vizuizi vingine vya kibiashara.

Hadi kufikia Juni 2025, kampuni 43 za Tanzania zimefanikiwa kuuza bidhaa zao Afrika kupitia mkataba huo, kwa kutumia vyeti 392 vya Uasili wa Bidhaa (Certificates of Origin) wakiuza bidhaa kwenye nchi zaidi ya 18 za Afrika ziikiwemo bidhaa za Nyuzi za katani kwenda Nigeria, Ghana, Morocco, na Misri; Vioo kwenda Misri; Mchele kwenda Burkina Faso na Cote d’Ivoire; na Kahawa kwenda Algeria.