Habari
Tanzania na Kenya Kuimarisha Uhusiano wa Kiuchumi
Tanzania na Kenya Kuimarisha Uhusiano wa Kiuchumi
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania, Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe, alisisitiza kuwa Tanzania na Kenya zitawndelea kuimarisha uhusiano thabiti na wa kudumu baina ya nchi hizo unaochangia kuongezeka kwa biashara na uwekezaji kwa kiwango kikubwa katika miaka ya hivi karibuni ambapo Kenya imekuwa ikileta bidhaa muhimu kama vile mafuta, vinywaji, na bidhaa za kilimo nchini, na Tanzania ikisambaza sukari, saruji, na mashine kwenda Kenya.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa usalama baina ya nchi hizo mbili, hasa katika kukabiliana na uhalifu wa kimataifa, uvuvi haramu, ujangili, na biashara ya dawa za kulevya kwa kutumia juhudi za pamoja za vyombo vya usalama vya mataifa hayo mawili katika kulinda usalama wa kikanda na utulivu.
Kigahe ameyasema hayo Disemba 13, 2024 wakati akitoa Salamu za dhati kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa Rais William Ruto na Wakenya wote, kwa kuadhimisha Siku ya Uhuru wa miaka 61 ya Kenya katika katika hafla maalumu iliyofanyika Dar es Salaam, Tanzania.
Aidha, Kigahe alitaja maendeleo makubwa ambayo Kenya imefanya katika sekta mbalimbali, ikijumuisha miundombinu, elimu, afya, na ukuaji wa uchumi yaliyotokana na Uongozi wenye maono wa Kenya ambao umechangia mafanikio.
Vilevile Kigahe amebainisha kuwa Tanzania na Kenya zitaendelea kushirikiana katika nyanja za utamaduni, utalii, elimu, na michezo hususani katika kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027,