Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Tanzania na Marekani kushirikiana Kibiashara katika Sekta ya Kilimo


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amekutana na kuzungumza na Afisa Tawala Huduma za Kilimo za mambo ya nje kutoka Idara ya Kilimo ya Marekani, Bw. Daniel B Whitley na ujumbe wake wakati wa Kongamano la 20 la AGOA Johannesburg, Afrika Kusini Novemba, 2023.


Dkt Abdallah amejadiliana na ujumbe huo kuhusu kuimarisha uhusiano wa kibiashara katika sekta ya kilimo kati ya Tanzania na Marekeni ikiwa ni sehemu ya Makubaliano ya Majadiliano ya Kibiashara kati ya Tanzania na Marekani yaliyosaini hivi Karibuni