Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Tanzania na Saudi Arabia zakubaliana kukuza biashara 


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Biashara wa Saudi Arabia Dkt. Majid Al Kasabi kuhusu kuendeleza uhusiano wa kibiashara na kuhakikisha mauzo ya bidhaa baina ya nchi hizo yanaongezeka. Kikao hicho kimefanyika tarehe 28 Aprili, 2024 sambamba na Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani Jijini Riyadh, Saudi Arabia