Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Tanzania na Uingereza kuwezesha wafanyabiasha baina ya nchi hizo kushirikiana


Tanzania na Uingereza kuwezesha wafanyabiasha baina ya nchi hizo kushirikiana

Waziri wa Viwanda na Biashara,Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema Tanzania na Uingereza zitaendelea kuimarisha uhusiano wake wa kibiashara hususani katika kuwawezesha Wafanyabiashara wa Nchi hizo kufanya biashara kwa ushirikiano.

Vilevile, amesema Nchi hizo zimekubaliana kushirikiana katika kutoa elimu ya jinsi ya kusafirisha bidhaa baina ya nchi hizo pamoja na kuwawezesha Wafanyabiashara wa Tanzania kusafirisha bidhaa zilizoongezwa thamani katika soko la Uingereza bila ushuru

Waziri Jafo ameyasema hayo Februari 20, 2025, baada ya kukutana na kuzungumza na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika Mhe. Lord Collins Aliyeambatana na ujumbe wake katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Dkt. Jafo amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha malengo ya wizara yake yanatimia na amesisitiza kuwa ili fursa hiyo itumike ipasavyo, nchi hizo zitashirikiana katika kutoa elimu kwa wananchi ili waifahamu na kunufaika nayo.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuongeza thamani katika bidhaa zinazouzwa nje na kuhakikisha zina ubora unaotakiwa kimataifa